Zingatia Haya Ubaki Ukiwa na Afya Ndani na Njeya Ramadhani

Zingatia Haya Ubaki Ukiwa na Afya Ndani na Njeya Ramadhani

Ramadhani ni mwezi wa Tisa katika miezi ya kiislam. Ndani ya mwezi huu waumini watiifu wa dini ya kiislam hufunga yaani hujizuia kula, kunywa na kukutana kindoa  kuanzia asubuhi(kabla ya machweo) mpaka jioni(baada ya mawio), pia hujiweka mbali na  upuuzi na maovu ya aina zote. Waislam wanaamini kuwa Funga huwasaidia kujifunza uvumilivu, adabu na kuongeza uchamungu.

Mabadiliko ya Mlo

Funga kwa kiasi kikubwa inabadilisha utaratibu mzima wa mlo, kwani ulaji ni baada ya jua kuzama na kabla ya asubuhi tu. Hii inaweza kupelekea kushuka metaboliki ya mwili (body metabolism) lakini, ulaji wa milo yenye virutubisho vya kutosha utakufanya ubaki mwenye afya njema.

Gawanya ulaji wako katika milo mitatu

  • Daku (saher) chakula kinacholiwa kabla ya jua kuchomoza asubuhi. Funga inaanza baada ya chakula hiki
  •  Futari(iftari) chakula wakati wa kufungulia Swaumu(funga) baada ya jua kuzama hiki ni chakula chepesi. Usishibe sana
  • Chajio (Dinner) masaa mawili hadi matatu baada ya kufuturu

Mambo ya Kuzingatia kwa Ulaji wa Afya Njema

  1. Kula vyakula vilivyo na fibres (nyuzinyuzi) za kutosha wakati wa Daku. Hivi ni vyakula vinavyopatikana katika nafaka na mbegumbegu mfano mtama, Matunda safi, mboga za majani na mkate wa nafaka zisizokobolewa. Unnashauriwa kunywa maji mengi Ili kupunguza gesi inayoweza kuletwa na vyakula vilivyo na nyuzinyuzi (fibres).
  2. Kwa kawaida Tende, Maji na juisi hutumika wakati wa Kufuturu. Tumia tende tatu na kama ml 120 ya juisi ili ikusaidie kurudisha sukari katika hali ya kawaida mwilini na kukupa nguvu ya haraka
  3. Chagua nyama zilizo na mafuta kidogo(lower fat). Ondoa ngozi ya kuku na mafuta yanayoonekana wazi kabla ya kupika kuku au nyama za aina nyingine.
  4. Oka au choma vyakula badala ya kuvikaanga, na kama utalazimika kukaanga punguza kiwango cha mafuta unayotumia. Pia pima mafuta kwa kutumia vijiko badala ya kumimina bila kupima wakati wa kupika.
  5. Kula taratibu na hakikisha unatafuna chakula vizuri kabla ya kumeza. watu wengi wana tabia ya kula chakula kingi kwa haraka hivyo kupelekea matatizo ya tumbo(indigestion) . Kumbuka inachukua hadi dakika 20 kwa tumbo lako kuujulisha ubongo kuwa umeshiba.
  6. Jenga tabia ya kutembea kwa angalau dakika 30 kila siku baada ya saa 1 hadi 2 baada ya futari. Kutembea kutasaidia mwili kubadiisha maji na chakula ulichukula kwa faida ya mwili (body metabolism). Ni vizuri chakula cha futari kikawa chepesi.
  7. Kunywa vinywaji kwa wingi kwa kadri uwezavyo(maji ni bora). Unashauriwa kunywa vikombe 8 hadi 12 kati ya futari na kabla ya kulala ili mwili uweze kurekebisha kiwango cha maji mwilini tayari kwa ajili ya swaumu ya siku inayofuata.


 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*