Jinsi ya kupika ndizi nyama za bizari

Unajua kupika Ndizi Nyama? Ndizi ni kati ya chakula cha wanga, ambacho kinakazi muhimu yakuupa mwili nguvu. Ndizi mbichi tunaweza kuzichemsha tu ni kitafunio kizuri, pia tunaweza kuziunga kwa aina tofautitofauti kwa nazi, kwa mafuta na namna nyingi kuongeza mvuto wa chakula chako. Sio siri mambo ya wiki nzima wali ugali vinachosha na kuondoa hamu ya chakula, basi weka nafasi ya vyakula vyengine kwenye ratiba yako, ndizi, viazi, kande, nakadhalika viwemo. Sasa leo tumeamua kuunga ndizi zetu kwa nazi, na bizari ikiwemo kuleta ladha na mvuto zaidi.

Pishi: Ndizi Nyama

Mahitaji

 • Nyama nusu
 • ndizi mbichi chana 3
 • nazi kubwa 2
 • mafuta nusu kikombe
 • pilipilimanga kijiko 1
 • bizari ya manjano kijiko 1 1/2
 • Pilipili hoho
 • karoti
 • kitunguu 2
 • vitunguu thoum
 • nyanya 6
 • tangawizi kiasi
 • chumvi kiasi

Jinsi ya Kupika Ndizi nyama hatua kwa hatua

 1. Katakata nyama, ioshe vizuri, itie vitunguu thoum, tangawizi ilosagwa na chumvi, kisha ibandike jikoni ichemke.
 2. wakati nyama inaendelea kuiva, andaa ndizi kwa kuzimenya na kuzikwangua kisha zioshe vizuri
 3. endelea kuandaa nyanya, vitunguu, karoti , hoho zako
 4. kuna nazi ichuje tui zito na jepesi lieke tofauti
 5. bandika sufuria, weka mafuta, yakipata moto kaanga vitunguu hadivibadilike rangi, tia thoum , endelea kukaanga kidogo kisha tia hoho nazo kaanga
 6. kisha weka nyanya endelea kukaanga, weka bizari yako koroga. Baada ya hapo mimina ndizi  zigeuzegeuze  zijikaange. Weka chumvi kwenye chakula chako, na weka ile nyama tulioichemsha na supu yake viendelee kuchemka na ndizi zetu.
 7. Weka tui  jepesi kwenye ndizi, tupia na karoti zako bila kusahau pilipili manga ilosagwa kwa ladha (ukipenda)
 8. Tui jepesi likisha chemkia vizuri na kupungua kwenye ndizi, tia tui zito na uache kiasi dakika 5 nalo lichemkie kisha epua ndizi zitakua tayari.

Haya wanajiko ndizi zetu tayari. Kitu cha muhimu kukumbuka katika upishi huu wa leo, tumia ndizi ambazo sio ngumu sana kuiva ili pale utapozikaanga hadi utapotia tui jepesi likachemka nazo ziwe zishaiva. Mi nimendaa na juisi ya tikitimaji na mapesheni, karibu.

 
 

No Comments

 1. Abely Charles Shilla says:

  Nashukuru kila siku najifunza kitu kipya ila naomba kufahamu Chuo kizuri cha mapishi pamoja na zana mpya za mapishi, mf kifaa cha kupambia keki,kaki za sambusa.

   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*