Jinsi ya kupika Pilau ya kuku

Jinsi ya kupika Pilau ya kuku

jinsi ya kupika pilau ya kuku: Habari za leo wapenzi wa blogu yetu hii ya Mapishi ya kiswahili. Leo tunakuletea pishi la chakula kipendwacho na wengi, Pilau ya kuku. Fuatana nami hatua kwa hatua namna ya kupika wali huu.

Jinsi ya kupika pilau ya kuku: Hatua kwa hatua

Mahitaji

 • Mchele wa basmati         kilo 1
 • Kuku                              ½
 • Viazi                               5
 • Vitunguu                          2
 • Thomu iliyosagwa             3 vijiko vya supu
 • Binzari ya pilau nzima       1 Kijiko cha chakula
 • Binzari ya pilau                 1 kijiko cha chai
 • Pilipili manga nzima           ½ kijiko cha chai
 • Karafuu nzima                    10
 • Iliki nzima                          8
 • Mdalasini nzima                 6 vijiti
 • Pilipili mbichi iliyosagwa     3
 • Chumvi                             kiasi
 • Mafuta ya kupikia              ¼ lita

 

Namna ya kupika pilau- Hatua kwa hatua

 1. Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
 2. Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha chemsha vipande vyako pamoja na chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
 3. Kuku akishawiva, mtoe weka kwenye bakuli safi, Bakisha supu katika sufuria.
 4. Tia mafuta kiasi katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi na kuwa ya hudhurungi.
 5. Tia thomu na tangawizi na binzari zote, kisha kaanga tena kidogo.
 6. Tia viazi katika mchanganyiko wako huo, kisha endelea kukaanga kidogo.
 7. Tia vipande vyako vya kuku na supu (iliyobaki wakati wa kupika kuku) katika mchanganyiko wako huo, acha ichemke kidogo kisha tia maji, kisia kutokana na mchele unaotumia.
 8. Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza).
 9. Ukishakuwa tayari pakua  kwenye sahani tayari kwa kula.

Pishi la pilau: Dondoo

Chakula hiki kinaweza kutosha mlo wa watu 3-4, unaweza kuongeza au kupunguza vipimo vya mahitaji kulingana na idadi ya walaji. Pilau ya kuku ni vizuri ikiliwa na salad na pilipili. Pia unaweza kushushia pamoja na juisi ya matunda. Natumai umefurahia pishi letu la leo waweza kutoa maoni yako hapo chini kuhusu jinsi ya kupika pilau ya kuku. Akhsanteni


 
Tags:

22 Comments

 1. lemmy matumba says:

  Asante kw ufundi wako umetukomboa kias kikubw sn kw upande Wa kna Dada much thanks ccter!!

 2. Asante Saha – namwaga mate

 3. Nimeipendaaaa pishiii zuri sana

 4. nicholaus magambo says:

  Nmependa xn uo upixhi wa pilau but lugha kidg inachanganya ungetumia lugh nyepec kidg ili kila Mt apate kuelewa

 5. daaaaa ver nyc

 6. samahani mi sijaelewa unaposema binzari ya pilau nzima, yaani una una maana kiungo hicho kinaitwa kwa jina hilo?

 7. MATILDA NIKATA says:

  ni nzuri nimeipenda

 8. rebecca willium says:

  mbona haujaelezea nyama ya kuku umeweka muda gani.

 9. Thanks so much but it will be more easier when you shoe the ingredients because some hatuzijui kama Thomu sijui nini.

  • Chef Rahma says:

   Thanks for your good advice Wanjiku, we ‘ll add special ingredient’s page with picture and explanations. thomu ni vitunguu swaumu (garlic)

  • Shukrani Sana Kwa maelezo hayo. Je, karafuu lazima itumike Kwa pamoja???

 10. Nimeipenda na nitajaribu kuipika. Naamini itakuwa poa

 11. Hellow ;samahani huo mchele wa bismati ni lazima kuutumia?alafu maneno mengine magumu kuyaelewa.samahani kwa usumbufu.punguza kidogo ukali wa maneno.

 12. lazima viungo vyote ulivyoandika hapo vitumike?

 13. Edith Kashula Lyaruu says:

  Mapishi ya pilau la kuku ni mazuri nimejifunza ila sijajua unaweza kutumia na mboga gani ya pembeni

  • Asante sana dada Edith, Pilau hilo unaweza kutumia na mboga yoyote ya majani kama chainiz, mchicha, kisamvu (cha karanga), n.k. tutaleta mapishi ya mboga hizo hivi karibuni, endelea kutembelea blogu yetu.

 14. Hapo naona mchele wa basmati
  oJe waweza tumia mchele aina nyingine? maana basmati haishikiki
  Asante

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*