Jinsi ya kupika wali wa manjano

Ni mara nyengine tena tukutane katika jiko letu. Leo wali, chakula kilozoeleka mno na watu wengi, lakini wali wetu sisi leo utakua na ladha nzuri zaidi na rangi tofauti, hivyo unavutia mlaji. Sio lazima wali uwe mweupe kila siku utachosha walaji. Karibuni sana tuandae chakula chetu.

Mahitaji

 • Mchele kilo 1
 • Mafuta nusu kikombe
 • Vitunguu maji 2
 • Vitunguu thoum kiasi
 • Chumvi kiasi
 • bizari ya manjano kijiko 1

Jinsi ya Kuandaa na Kupika Wali wa Manjano Hatua kwa Hatua

 1. Chambua mchele vizuri, upete na uukoshe
 2. bandika sufuria, tia mafuta, wacha yapate moto
 3. tia vitunguu uvikaange, kisha vitunguu thoum na binzari, endelea kukaanga kidogo
 4. mimina mchele na chumvi, uchanganye vizuri
 5. Ongeza maji ya moto, changanya vizuri, funika uuache uendelee kuiva na kukauka maji
 6. maji yakikauka, angalia kama umeshaanza kuiva, kama tayari upalie moto juu na chini ukauke vizuri. Ukisha kauka wali wetu utakua tayari, waweza upakua

Wali wa manjano waweza liwa na mchuzi, kachumbari, kitoeo, matunda na hata juisi upendayo. karibuni sana.

 
 

No Comments

 1. maida says:

  Naupenda. Sana wali wa manjano asante kwa kutufunza nazan tutakuwa wapish bora kwa familia zetu

   
 2. Grace Lunyaba says:

  asante sana kwa kuwa pamoja na sisi

   
 3. abigael says:

  mi sijaelewa kuhusu binzari ya kutia kwenye wali, ni binzari yoyote tu au inaitwa binzari ya wali? msaada tafadhali

   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*