Ni yepi Madhara ya Chumvi?

Ni yepi Madhara ya Chumvi?

Habari ndugu yangu,msomaji wa Blogu yeko hii. Leo ninakuletea dondoo kidogo kuhusu Matumizi na madhara ya chumvi. Kwa miaka mingi chumvi imeendelea kuwa kiungo muhimu katika chakula cha binaadamu, ukitaka kujua umuhimu wa chumvi pika mboga nzuri halafu usitie chumvi!

Je miili yetu inahitaji chumvi?

Chumvi ina madini (sodium) ambayo husaidia miili yetu kuwa na maji ya kutosha-yaani siyo maji mengi kupita kiasi wala siyo kidogo kupita kiasi. Kwa hiyo tumia chumvi kidogo tu katika chakula wakati wa kupika au kula mezani.

Vilevile, kama utakula mchanganyiko wa kutosha wa vyakula, huna haja ya kuongeza chumvi unapopika au unapokula mezani.

Ni kwanini utumie chumvi kidogo tu?

Chumvi ikizidi mwilini husababisha mrundikano wa maji mwilini. Hivyo unapokula chumvi nyingi unaweza kupata madhara kiafya. kwa mfano:

 • Shinikizo la damu mwilini kuwa kubwa kupita kiasi
 • Magonjwa ya moyo
 • Kiharusi yaani, kupooza kunakosababishwa na shinikizo la damu kuwa juu sana
 • Kuharibika kwa figo
 • Maradhi ya mifupa
 • Saratani ya tumbo
 • kupoteza uwezo wa macho kuona

Je utumie kiasi gani cha chumvi kwa siku?

Mashirika mengi ya Afya ulimwenguni yanapendekeza matumizi kidogo ya chumvi (Sodium) kama ifuatavyo

 • United States Department of Agriculture (USDA): 2300 miligramu (1).
 • American Heart Association (AHA): 1500 miligramu (2).
 • Academy of Nutrition and Dietetics (AND): 1500 mpaka 2300 miligramu (3).
 • American Diabetes Association (ADA): 1500 mpaka 2300 miligramu.

Kiasi kinachofaa kwa mujibu wa wataalamu wa Afya ni miligram 2300 sawa na kijiko kidogo cha chai kwa siku. Na kwa watu wenye shinikizo la damu wasizidishe miligramu 1500 sawa na 3/4 ya kijiko cha chai kwa siku.

Kiasi kinachofaa kwa matumizi ya chumvi kinatofautiana kutokana na Hali ya kiafya, Umri, na Kazi ya mtu. Hivyo ni bora kumuona daktari wako akushauri kiasi kinachofaa kwa afya yako binafsi.

Hayo ndiyo madhara ya kutumia chumvi nyingi. Je una taka kutujuza chochote kuhusu madhara ya chumvi? Maoni yako yanakaribishwa hapo chini. Asante


 

One Comment

 1. mkemia Ndonde says:

  Je nitaijuaje chumvi mbovu au nzurii?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*