Jinsi Ya Kupika Bagia za Kunde na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA BAGIA ZA KUNDE

Jinsi ya kupika bagia za kunde na mapishi ya bagia za kunde pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika bagia unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Bagia za Kunde

1. Vikombe 2 kunde

2. Kitunguu 1 kikubwa

3. Pilipili kichaa 2 (nyekundu na kijani ukipenda)

4. Vijiko 3 vya chakula maji ya limao (ukipenda)

5. Kijiko 1 cha chai baking powder

6. Vijiko 1½ vya chai tangawizi

7. Kkombe ¼ majani ya giligilani

8. Chumvi kwa kuonja

9. Mafuta ya kukaangia️

JINSI YA KUPIKA BAGIA ZA KUNDE

1. Osha na kuloweka kunde kwenye maji ya moto siyo chini ya masaa 8, au usiku mzima

2. Katakata kitunguu, pilipili, majani ya giligilani; twanga tangawizi. Weka pembeni

3. Chuja kunde maji

4. Weka kunde, maji ya limao na pilipili kwenye mashine ya kusagia chakula au blender ila isilainike sana.

5. Unaweza pia kutumia mashine ya mkono ukipenda au kutwanga kwenye kinu. (hakikisha mashine yako ina nguvu ya kutosha kusaga kunde)

6. Ikilainika, ongeza kitunguu na majani ya giligilani kwenye mchanganyiko, saga kwa sekunde kama 20.

7. Hakikisha vitunguu na majani ya giligilani hayasagiki kabisa.

8. Weka mchanganyiko kwenye bakuli kubwa.

9. Ongeza chumvi na baking powder, changanya vizuri

10. Chemsha mafuta kwenye kikaango katika moto wa wastani.

11. Yakichemka, tumia vijiko 2 au mikono kutengeneza umbo kama la yai au umbo la bagia

12. Weka kwenye mafuta. Kaanga mpaka ziwe na rangi ya kahawia

13. Toa bagia zilizoiva kwenye mafuta.

14. Hamishia kwenye sahani au bakuli iliyowekewa tissues, au tumia chujio la bati ili mafuta yajichuje.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply