Jinsi Ya Kupika Cake Laini na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA CAKE LAINI

Jinsi ya kupika cake laini kwa kutumia oven na mapishi ya cake tamu pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika cake unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes Za Jinsi Ya Kupika Cake

1. Siagi Kikombe 1

2. Sukari Kikombe 1

3. Unga Vikombe 2

4. Maziwa 1/2 (nusu) Kikombe

5. Mayai 4

6. Baking Powder 1 Kijiko cha supu

Mapishi Ya Kupika Cake Kwa Kutumia Oven

1. Washa oveni 350 – 400 Deg C liache lishike moto huku ukitayarisha mchanganyiko wa keki.

2. Changanya sukari na siagi mpaka ichanganyike.

3. Mimina mayai na maziwa uchanganye vizuri.

4. Mimina Baking Powder kwenye unga na uchanganye vitu vyote pamoja.

5. Endelea kuchanganya vizuri mpaka uhakikishe vimechanganyika vizuri (unaweza kufanya bila ya mashine)

6. Chukua trey ambayo haitojaa ukiimimina, ipake siagi na umimine mchanganyiko wako. Treya isiwe nzito sana au nyepesi sana bali iwe wastani.

7. Ipike (Bake ) mpaka iwive na itakuwa cake laini na tamu.

8. Epua iache ipoe ndio ukate kate vipande.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply