Jinsi Ya Kupika Chapati za Maji na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA MAJI

Jinsi ya kupika chapati za maji na mapishi ya chapati za maji pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika chapati za maji unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Chapati za Maji

1. Ngano ½ kilo

2. Mayai 3

3. Mafuta ¼ kikombe

4. kitunguu kikubwa kilichosagwa 1

5. Kitunguu Swaumu punje 4

6. Chumvi ½ kijiko au zaidi kulingana na matakwa yako

Jinsi Ya Kupika Chapati za Maji

1. Chekecha unga wako wa chapati vizuri weka katika bakuli safi.

2. Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito sana wala si mwepesi sana.

3. Ongeza mayai na chumvi endelea kukoroga.

4. Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto.

5. Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili.

6. Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza chapati yako mpaka iwe rangi ya kahawia.

7. Hapo utakuwa umemaliza jinsi ya kupika chapati na zitakua tayari kwa kuliwa Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply