Jinsi Ya Kupika Chapati za Viazi na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA VIAZI

Jinsi ya kupika chapati za viazi na mapishi ya chapati tamu za viazi pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika chapati za viazi unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

RECIPES ZA JINSI KUPIKA CHAPATI

DONGE LA CHAPATI

  1. Unga wa ngano vikombe 4
  2. Mafuta viJiko 2 chakula
  3. Maji kiasi
  4. Siagi ½ kikombe

UPANDE WA VIAZI VYA CHAPATI

  1. Viazi vilivyochemshwa na kupondwa 4
  2. Chumvi kiasi
  3. Binzari ya unga ½ kiJiko chai
  4. Pilipili ya unga ½ kiJiko chai/ukipenda
  5. Kitunguu kilichokatwa katwa 1

MATAYARISHO NA JINSI YA KUPIKA

1. Changanya mahitaji yote ya unga kisha kanda kufanya unga mlaini.

2. Funika acha ukae ½ saa, fanya madonge size upendayo.

3. Changanya mahitaji yote ya viazi weka pembeni.

4. Chukua donge moja sukuma kufanya chapati ndogo, chota mchanganyiko wa viazi kisha funika vizur na zungusha kufanya donge tena. Rudia kwa madonge yote.

5. Sukuma chapati zako na choma kama kawaida katika moto wa kiasi hadi zipate rang nzuri.

6. Chapati za viazi tayari kwa kula na curry yoyote.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply