Jinsi Ya Kupika Cupcake na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA CUPCAKE ZA BIASHARA

Jinsi ya kupika cupcake na mapishi ya cupcake pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika cupcake unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Cupcake

1. Siagi ¾ kikombe

2. Sukari kikombe 1½

3. Mayai 2

4. Vanilla viJiko 2 chai

5. Baking powder viJiko 2½ chai

6. Chumvi ¼ KiJiko chai

7. Unga wa ngano vikombe 2½

8. Maziwa ya maji kikombe 1¼

JINSI YA KUOKA CUP CAKE

1. Washa oven joto 175°c. Tia paper liners katika muffin tins au paka mafuta kila tundu la muffin tray.

2. Katika bakuli chekecha unga, chumvi pamoja na baking powder, koroga kuchanganya vizuri kisha weka pembeni.

3. Katika bakuli piga siagi hadi iwe laini, tia vanilla na sukari kisha piga tena hadi mchanganyiko uwe mweupe.

4. Tia yai moja baada ya jingine ukipiga vizuri kila unapotia.

5. Kwa kutumia mwiko au spatula tia unga taratibu pamoja na maziwa,ukianza na kumaliza na unga.

6. Mimina katika muffin tins kisha oka hadi zipate kuwa rangi ya brown.

7. Acha zipoe kabisa katika wire rack, Kisha Unaweza KuPambia kwa icing uipendayo.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply