Jinsi Ya Kupika Doughnut Laini na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA DOUGHNUT LAINI

Jinsi ya kupika doughnut na mapishi ya doughnuts pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika doughnut unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Doughnut

1. Unga wa ngano kilo 1

2. Mafuta ya kupikia donati lita 1

3. Sukari iliosagwa robo kilo

4. Hamira

5. Siagi

6. Maziwa robo lita

7. Mdalasini ulosagwa

8. Mayai 3

9. Baking powder kijiko 1 kikubwa

Jinsi Ya Kupika Dougnut

1. Changanya unga na baking powder pamoja na siagi hadi unga uchanganyike tia sukari kidogo, kungumanga na yai kisha endelea kuchanganya unga.

2. Weka maziwa na kanda mpaka upate donge laini tengeneza madonge, uanze kusukuma unga kiasi cha sentimeta moja. Usiwe mwembamba sana kama wa chapati.

3. Kata duara la doughnut kwa glasi au kikombe kisha kata duara lingine dogo katikati kwa kutumia kifuniko cha chupa ya maji au kitu chochote chenye duara dogo, upate shepu ya ringi.

4. Bandika mafuta jikoni, yakipata moto tia donati uzikaange mpaka ziwe na rangi nzuri ndipo uzitoe jikoni doughnuts zako.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply