Jinsi Ya Kupika Kababu za Nyama na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA KABABU ZA NYAMA YA KUSAGA

Jinsi ya kupika kababu za nyama ya kusaga na mapishi ya kababu za nyama pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika kababu za nyama ya kusaga unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Kababu za Nyama Ya Kusaga

1. Nyama ya kusaga Kilo 1

2. Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa Kijiko 1 cha chai

3. Pilipili mbichi iliyosagwa kijiko 1 cha chai

4. Bizari ya Kababu ½ paketi

5. Chumvi kiasi

6. Mafuta kiasi ya kukaangia

7. Mayai 2

8. Slice 2 za Mkate

JINSI YA KUPIKA KABABU ZA NYAMA

1. Weka nyama Yako katika bakuli kubwa

2. loweka slice za mkate katika maji kisha zikamue maji uzivuruge kwa mkono ndani ya nyama hakikisha zinachanganyika na nyama vizuri

3. Changanya nyama pamoja na viungo vyote katika bakuli.

4. Chukuwa mayai yako vunjia katika huo mchanganyiko changanya tena mpaka vichanganyike

5. Fanya madonge shape ya duara kama kwenye picha weka kando.

6. Kisha Kaanga kama sambusa mpaka Zibadilike rangi.

7. Epua zikiwa tayari kwa kuliwa.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply