Jinsi Ya Kupika Kashata za Karanga na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA KASHATA

Jinsi ya kupika kashata na mapishi ya kashata pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika kashata unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Kashata za Karanga

1. Karanga – ½kg

2. Sukari ya Brown – ½kg

3. Maji – ¼ Cup

4. Siagi – 1 KiJiko

JINSI YA KUPIKA KASHATA ZA KARANGA

1. Pasha sufuria jikoni kwa moto wa wastani. Zikaange karanga kwa dakika 4 – 5 kaanga hadi ziive, kuwa makini zisiungue kuwa nyeusi.

2. Zikiiva zitoe jikoni wacha zipoe toa maganda ili ziwe nyeupe.

3. Tumia moto mdogo na weka sufuria jikoni tia sukari na maji. Koroga taratibu hadi sukari na maji kuchanganyika na kunata huchukua kama dakika 6-7.

4. Mimina karanga kwenye mchanganyiko wa maji na sukari, changanya vizuri kwa dakika chache na zima jiko.

5. Pakaza sahani siagi na mimina mchanganyiko. Kisha tandaza vizuri wacha ipoe kwa dakika muda kidogo.

6. Kisha kata vipande ikiwa ya moto moto. Weka sehemu ya ubaridi ili kuganda. Baada ya hapo Kashata za karanga zitakuwa tayari kuliwa.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply