Jinsi Ya Kupika Maharage Kwa Kutumia Chupa Ya Chai

JINSI YA KUPIKA MAHARAGE

Jinsi ya kupika maharage na mapishi ya maharage kwa kutumia chupa ya chai pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukala na chakula kingine chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika maharage unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

JINSI YA KUPIKA MAHARAGE KWA CHUPA YA CHAI

Kuna njia mbali mbali za kupika maharage lakini kuna moja haitambuliki sana na watu wengi ingawa inahitajika mpishi awe na subira pale anapotumia mbinu hiyo.

Unachohitaji kuwa nacho ni Chupa ya chai au Thermos Flask pekee na utapika maharage mpaka yaive kwa njia nyepesi na bora zaidi.

HATUA ZA JINSI YA KUPIKA

1. Kwanza, tafuta chupa ya chai (Thermos Flask) ambayo itakuwa na ukubwa sawa na maharage unayotaka kupika.

2. Pima kiwango cha maharage unachohitaji kwa kutumia kikombe.

3. Chemsha maharage hayo kwa muda mfupi kwenye sufuria.

4. Kisha yaweke kwenye chupa yako ya chai

5. Yaache kwa muda wa masaa sita kama ni usiku yaache yalale ndani ya chupa hiyo.

6. Baada ya hapo, maharage yako yatakuwa yanafaa kupikwa vizuri kwa viungo (Kuungwa) kwa ajili ya Kuliwa

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply