Jinsi Ya Kupika Tambi za Unga wa Dengu na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA TAMBI ZA DENGU

Jinsi ya kupika tambi za unga wa dengu na mapishi ya tambi za dengu pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika tambi za dengu unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Tambi

1.    Unga wa dengu ½ kilo

2.    Binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani

3.    Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai

4.    Unga wa mchele ¼ kilo

5.    Chumvi kiasi

6.    Mafuta ya kula ½ lita

7.    Baking powder

Jinsi Ya Kupika Tambi za Dengu

1. Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga.

2. Baada ya hapo changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukiukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja.

3. Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa.

4. Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni.

5. Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka tambi zako zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Epua na weka pembeni. Weka tambi kwenye sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply