Jinsi Ya Kupika Ubuyu Mtamu na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA UBUYU

Jinsi ya kupika ubuyu mtamu na mapishi ya ubuyu wa zanzibar pamoja na recipe yake pia ubuyu huu ni mzuri kwa matumizi ya nyumbani na kwa biashara

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika ubuyu unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Ubuyu

1. Sukari vikombe 2

2. Maji vikombe 2

3. Nusu kikombe unga wa ubuyu

4. Vikombe 4 ubuyu wenyewe

5. Kijiko ¼ cha pili pili ya unga

6. Kijiko ¼ cha chumvi

7. Kijiko ¼ cha iliki ya unga

8. Rangi nyekundu au yeyote utakavyopenda.️

JINSI YA KUPIKA

1. Katika sufuria,weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.

2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri.

3.Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito. Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu.

4. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.

5. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung’aa na kushika vizuri katika ubuyu.

6. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply