Jinsi Ya Kupika Vitumbua Laini Vya Mchele na Mapishi Yake

JINSI YA KUPIKA VITUMBUA LAINI

Jinsi ya kupika vitumbua na mapishi ya vitumbua pamoja na recipe yake pia chakula hiki ni kizuri sana na unaweza ukashushia na kinywaji chochote.

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kupika vitumbua unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Jinsi Ya Kupika Vitumbua

1. Mchele kilo 1

2. Nazi kubwa 2

3. Hiliki kiasi

4. Sukari robo kilo

5. Hamira kiasi kijiko kimoja nusu (itategemea aina ya hamira)

6. Mafuta nusu lita

Jinsi Ya Kupika Vitumbua

1. Uloweke mchele uliokwisha uchambua vizuri na kuupeta

2. Utandaze sehemu safi ukauke, kisha usage upate unga mlaini wa vitumbua

3. Kuna nazi uchuje tui zito

4. Saga hiliki, changanya na sukari

5. Changanya ule unga wa mchele, sukari, hiliki, tui la nazi na hamira. uvuruge uwe mwepesi kiasi cha kuweza kuchoteka kwa upawa.

6. Acha uumue kwa dakika 25 hadi 30 kutegeme na ubora wa hamira.

7. Weka kikaango cha kukaangia vitumbua jikoni, anza kukaanga vitumbua vyako kwa kuweka mafuta kwanza yapate moto, kisha unachota kwa upawa unga na kuweka kwenye vijungu vya kikaangio chetu.

8. Acha vitumbua vichemke upande mmoja, kisha unageuza upande wa pili, vikishaiva vitoe weka kwenye chujio ili mafuta yajichuje.

9. Endelea kukaanga viliobakia mpaka unga uishe.

10. Ukivipata vya moto moto na chai pembeni vitakukosha sana

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply