Jinsi Ya Kutengeneza Peanut Butter

JINSI YA KUTENGENEZA PEANUT BUTTER

Jinsi ya kutengeneza peanut butter au siagi ya karanga pamoja na recipe yake pia peanut butter hii ni nzuri sana na inakaa kwa muda mrefu bila kuharibika

Ukiwa na maelezo mengine mazuri zaidi ya jinsi ya kutengeneza peanut butter unaweza kunitumia ili niweze kuweka kwenye website yetu ya Jinsi Ya Kupika.

Recipes za Kutengeneza Peanut Butter

1. Karanga vikombe 2

2. Asali au sukari kijiko 1 na nusu cha chakula

3. Mafuta ya kupikia kijiko 1 na nusu cha chakula

4. Chumvi ½ kijiko cha chai

Jinsi Ya Kutengeneza Peanut Butter

1. Kaanga karanga bila mafuta mpaka zikaangike vizuri yani maganda yaanze kutoka yenyewe

2. Ziache zipoe kisha toa maganda

3. Mimina karanga, chumvi na mafuta katika blender ama food processor saga hadi iwe laini

4. Ongeza asali, chumvi, sukari au asali na mafuta saga hadi iwe laini

5. Hifadhi katika chupa yako kisha weka kwenye FriJi

Sisi Jinsi Ya Kupika Tunakuomba Utuandikie Mawazo Yako

Leave a reply