Jinsi ya kutengeneza biskuti za Ufuta

Jinsi ya kutengeneza biskuti (biscuit) za ufuta: Nimechagua kupika biskuti hizi kwa sababu kuu mbili. Kwanza ni rahisi sana kutengeneza na hazihitaji viungo vingi (mahitaji yake ni machache), Pili ni tamu sana. Nafikiri na wewe utazipenda.

Pishi: Biskuti za ufuta

Maandalizi na Mahitaji

Mahitaji

 • Unga wa ngano gramu 450 (kama vikombe 3 vya vya chai)
 • Sukari ya kusaga 1/4 Kikombe
 • Siagi 250 gramu (kama kikombe 1 na nusu)
 • Mayai 3
 • Jam kiasi
 • Ufuta gramu 120 (kama 3/4 ya kikombe)
 • Vanilla 1 kijiko cha chai

jinsi ya kupika

Directions

 • Changanya Siagi na sukari kwa kutumia Blenda au machine ya kutengenezea keki. Hakikisha imechanganyika vizuri.
 • Ongeza yai moja huku ukiendelea kuchanganya, kisha ongeza vanilla.
 • Tia mchanganyiko wako katika bakuli safi, Tia baking powder, na unga na changanya kwa mkono vizuri.
 • Paka siagi chombo (sinia) ya kupikia ya oveni.
 • Tengeneza viduara vidogo vidogo.
 • Bonyeza katikati ya kila kiduara kwa kidole, kisha weka jam, halafu juu yake paka mayai na unyunyuzie ufuta.
 • Pika katika moto wa chini 350ºF kwa muda wa dakika 20-25.
 • Tayari kwa kuliwa.

My rating 4 stars:  ????? 10 review(s)

Biskuti za ufuta: Dondoo
Waweza kutengeneza miundo mbalimbali kama pembe tatu, kopa nk kulingana na ubunifu wako

Hivi ndivyo kwa ufupi namna ya kutengeneza Biskuti za ufuta ningependa kusikia kutoka kwako, weka maoini yako hao chini

 

 

 
 

No Comments

 1. Fatma says:

  kwa kweli nimelike chef wangu

   
 2. cuttymafjuh says:

  ahhhh jamani yaani hakika nashkuru juu ya uwepo wa blog hii inanizidishia upeo wa kujua vyakula mbalimbali ila tuzingatie saana juu ya sawala la moto kama sehemu uliopo moto wake ukoo mkubwa punguza kidogo isifike 350`f kwa wale ambao umeme kwao uko kawaida unaweza kutumiaa. %(mwanamkee mapishiiii na sio ugombanishiiiii)%

   
 3. Mlaga says:

  Nimependa kujaribu kupika izo biskuti ila swali langu je kwa sisi ambao hatuna ovena hatuwezi kutumia majiko ya mkaa kwa kukadiria moto wa wastani?

   
 4. eliza says:

  Ahsante kwa pishi zuri nimelifurahia, nitajitahidi ili nijaribu kulipika

   
 5. ndimyake says:

  NIMEPENDA PISHI LAKO ASANTE KWA KUNIFUNDISHA NITAPIKA NA MIMI

   
 6. Mariam says:

  nadhani umesahau kuweka baking powder kwenye mahitaji kwa sababu kwenye maelezo umeitaja. Lakini nashukuru kwa pishi hili nilinunua ufuta mwingi na nilkua natafuta pishi la ufuta

   
 7. Beatha audax says:

  Na beking pouder unaweka kiasi gani

   
 8. neema moro says:

  biskuti hizi tamu sana

   
  • Salma Chef says:

   Endelea kufurahia Mapishi yetu. asante

    
 9. asmahan says:

  Nikitamu sn

   
 10. lizbeth says:

  Ufuta unawekwa kwenye atua gani???

   
 11. Neema Julius says:

  Wow ningependa kijaribu

   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*