Jinsi ya kupika keki ndogo za rangi

Jinsi ya kupika keki ndogo za Rangi na Icing: Zulfa ni Mwanafunzi wa Chuo fulani Jijini Dar es salaam na ni mpenzi mkubwa wa blogu hii.

Leo anatuletea pishi la keki fuatana nae…

Katika vyakula ambavyo napenda nipate walau mara moja kwa mwezi ni Keki. Nilipokuwa mdogo bibi yangu ambaye alikua akifanya kazi za ndani kwa wahindi alinifundisha mapishi mbalimbali. Moja ya mapishi hayo ni keki hii ninayoiandika sasa, Nimeviita vikeki kwa sabau ni vidogo vidogo na vinatoka vingi katika mpiko mmoja.

Jinsi ya kupika keki ndogo za icing; Hatua kwa hatua

Mahitaji

 • Unga wa ngano                              Kikombe kimoja na nusu
 • Maziwa                                             Robo Tatu ya Kikombe
 • Siagi isiyo na chumvi               Nusu Kikombe
 • Hamira (Bakin powder)         Kijiko kimoja cha chai
 • Chumvi                                          Nusu Kijiko cha chai
 • Sukari                                              Kikombe Kimoja
 • Mayai                                               3
 • Vanilla                                              Kijiko Kimoja na nusu cha chai

Namna ya Kutengeneza keki hatua kwa hatua

 1. Kwanza washa tanuri (oveni) kwa kiasi cha nyuzi joto 350°. Kisha weka karatasi za kupikia keki za vikombe kwenye trei.
 2. Tia Unga, Baking powder na chumvi katika Bakuri safi, halafu Changanya pamoja na uuweke kando mchanganyiko wako huo.
 3. Tia siagi na sukari katika bakuli la mashine changanya hadi ilainike vizuri.
 4. Wakati mchanganyiko wa siagi na sukari ukiendelyea kulainika, tia yai moja baada ya jingine huku unaendelea kuchanganya, halafu tia vanilla.
 5. Huku unaendelea kuchanganya, tia nusu ya mchanganyiko wa unga uliyoweka kando (katika hatua ya pili juu),
 6. kisha tia maziwa na umalizie na mchanganyiko wa unga uliyobakia.
 7. Ikisha changanyika vizuri, mimina kwenye karatasi za kuchomea keki za vikombe. Hakikisha usijaze mpaka juu.
 8. Weka katika oveni acha iive kwa muda wa kama dakika ishirini.
 9. Ziache zipoe. Zikisha poa zipake icing/cream upendayo na keki zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Mapishi ya keki hii: Dondoo

Utayarishaji huu unaweza kutoa keki ndogo 12. Waweza kuongeza au kupunguza kulingana na mahitaji yako

Hivyo ndivyo jinsi kupika Keki(vikeki) ndogo za Icing. usisite kutoa maoni hapo chini. Asante!

 
 

No Comments

 1. GAudencia makoba says:

  Unatumia mayai mangap kwa kipimo hicho

   
  • GAudencia makoba says:

   Ooh nshapata jibu

    
 2. eliza fabi says:

  da iz xo nice 100%

   
 3. eliza fabi says:

  nahitaji kujua zaidi kupika keki

   
 4. karima mustafa says:

  mie naitaji unielekeze kupika keki za biashara ila natumia kuni na mkaa oven sina nifanyeje ili ziwe na mvuto?

   
 5. Fahima bint nuru says:

  Je, kama auna jiko la umeme uwezi ku2mia la mkaa au gas?

   
 6. bupe says:

  Je ni karatasi za namna gani nitakazo weka kwenye vikombe ?

   
 7. Mariam says:

  Asante kwa pishi hili. Wiki iliyopita nilipika keki ya carrots ikatoka vizuri. Week-end hii nitajaribu vikeki hivi

   
 8. mary says:

  Natamani kujua kwa wasio na oven inakuwaje?

   
 9. silvia salema says:

  i’m really happy to know all these but the problem is that i have no an oven

   
  • Chef Rahma says:

   Sorry to hear that Silvia! ‘ll show how to bake cake without an oven on our upcoming courses…

    
 10. mory irs says:

  Thx…ila tunaomba option nyingine kwa wasio name oven

   
 11. hidaya says:

  Je ni karatasi za aina gani zinatumika

   
 12. mwema says:

  nimekuelewa sna ! nahitaji kujua jinsi ya kupamba keki

   
 13. lilian says:

  mimi nachanganya vizur ila inatoka mbichi au ungA ninao tumia

   
  • Mama Keki says:

   Tumia unga wa keki wa Azam au Ppf…. Unga wa kawaida wa ngano hutoa keki mbichi

    
 14. mzava says:

  tunahitaji video

   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*