Jinsi ya Kuandaa Kuku wa Kujaza

Jinsi ya Kuandaa Kuku wa Kujaza

Kuku wa Kujaza: Kuku ni moja kati ya kitoweo kipendwacho na wengi, kuku kitoweo, vitumbua, mboga, mchuzi, supu, yote mapishi yake. Leo tunaandaa kuku wa kujaza ambaye kwa jina jengine huitwa kuku wa mahshai. Tunamuandaa mzima bila kumkatakata, tunatoa vitu vyake vya ndani, tunamtengeneza na kisha tunamjaza wali, ni zuri hili pishi hivyo nakusihi usiende mbali na jiko letu.

Mahitaji

 • Kuku mkubwa 1
 • mafuta lita 1
 • mchele nusu kilo
 • vitunguu nusu kilo
 • tangawizi kiasi
 • thoum na uzile kiasi
 • hiliki na zabibu kidogo
 • chumvi vijiko 2

Kuandaa Kuku wa Kujaza hatua kwa hatua

 1. Chukua kuku aliyekwisha nyonyolewa vizuri na kutolewa vitu vya ndani, bila kumkata vipande mchemshe kwa maji na chumvi, mtie vitunguu, thoum, tangawizi na uzile ( viungo vyengine vibakishe).  Mwache achemke pamoja na hivyo viungo mpaka maji yakauke.
 2. Weka mafuta kwenye sufuria jikoni, umkaange kuku wako mpaka awe mwekundu. Kisha muepue muweke pembeni
 3. Bandika sufuria, itie mafuka kiasi kiaha kaange vitunguu kidogo, kisha tia thoum na viungo vyote vilivyobakia ukaange
 4. Chemsha mchele utie na chumvi, uuache uive kiasi. Kisha uchuje maji yote. Uchukue uutie kwenye ile sufuria yenye viungo tuliovikaanga ukoroge pamoja hadi ukauke. Fukua kidogo kati utie zabibu kavu, kisha uupalie kama wali wa kawaida
 5. ukishakuwa tayari wali, upakue uutie kwenye tumbo la kuku kisha umshikize kwa uzi mwembamba ili wali usitoke, hapo mueke kwenye sahani umpambe uwezavyo kwa saladi na mbogamboga. Kuku wetu tayari.

   

Kuku wetu wa kujaza tayari, na sio lazima umjaze wali mweupe, waweza kumjaza wali wa njegere, pilau, wali wa karoti, wali wa manjano na hata chipsi. Natumai tumefaidika na somo la leo namna ya kuandaa kuku wa kujaza, karibuni sana.


 
Tags:

17 Comments

 1. Wow, nimepanda pishi hili nitapika tule na familia pamoja marafiki zangu asante sana nimeelewa.

 2. Asante nimefaham

 3. Nimefurahia upishi wa kuku, maana napenda sana vyakula vitamu na vya chumvi km hivyo

 4. Nimependa upishi nilikuwa najiuliza vipi inapikwa hiyo kuku nimefurahi kupata upishi shukran sana

 5. maoni cna ila ushanitamanisha naenda kuupika leo

 6. Faith Kanyiva says:

  Napenda kupika sana nitajaribu f

 7. Mashallah

 8. suma mwampulo says:

  nashukuru kwa pishi zuri sana, ila naomba nifafanulie uzile ni nini na inapatikana wapi?

  • Salma Chef says:

   suma, uzile ni bizari nyembamba kwa jina jengine, yapatikana kunakouzwa viungo viungo kama mdalasini, hiliki n.k

 9. asante sana nimeipenda nami nitaandaa

 10. nimeipenda sana hiyo nami nitapika J’pili hii

 11. sini tamu……….ahsante.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*