Jinsi ya kupika Bamia na Karanga

Jinsi ya kupika Bamia na Karanga: Umewahi kula ugali kwa bamia? unajua namna ya kuandaa bamia tamu na karanga? Leo nimewaandalia pishi hili la kiswahili la kiasili, Tuwe pamoja

Pishi: Bamia na karanga

Maandalizi na Mahitaji

Mahitaji

 • Bamia mbichi
 • Kitunguu maji
 • Karanga zilizo kaangwa
 • Nyanya
 • Binzari
 • Vitunguu swaumu
 • Chumvi kidogo
 • Maji ya kutosha
 • Limau au ndimu

jinsi ya kupika

jinsi ya kupika bamia na karanga hatua kwa hatua

 1. Andaa karanga kwa kuzikaanga na kisha kuzitwanga au kusaga ili kupata unga
 2. Safisha na pauza/kwangua bamia, kata sehemu kidogo za mwisho na zitupe shambani ziwe mbolea. Zikatekate bamia vipane vidogo vidogo
 3. Menya nyanya kuondoa maganda kama ni lazima au sivyo osha nyanya katakata vpande vidogo vidogo pamoja na maganda yake
 4. Weka bamia, vitunguu, nyanya, binzari na chumvi kwenye chungu au sufuria. weka maji yanayocheaka ya kiasi tu.
 5. Bandika jikoni, endelea kupika mpaka mchanganyiko uive kidogo (dakika 10). Ongeza matone machachae ya limao au ndimu.
 6. Changanya maji kidogo ya moto na karanga, ongeza kwenye chugu au sufuria yenye bamia.
 7. Endelea kupika kwa moto mdogo kwa dakika tano huku ukiendelea kukoroga kila mara. Ongeza maji ya moto kama yanahitajika.
 8. Hakikisha mboga na karanga vimeiva na karanga hazikuungulia kwenye kitako cha sufuria au chungu
 9. Epua na andaa tayari kwa kuliwa

Pishi la bamia na karanga: Dondoo

 • Kwa kuongeza mvuto wa mboge yako waweza tupia pilipili nyekundu, korosho kama 8
 • Kuongezea ladha waweza kuweka maziwa ya mgando(mtindi) wakati unapika.
 • Waweza kula mboga ya bamia pamoja na Ugali wa mahindi, muhogo au mtama.

Natumai umefurahia jinsi ya kupika bamia na karanga, Asante

My rating 5 stars:  ????? 1 review(s)

 
 

No Comments

 1. eliza says:

  ahsante kwa pishi zuri

   
 2. Eng Chief Mtwe says:

  Ni nzuri

   
 3. adela mwampamba says:

  leo nimejaribu kupika ikawa tamu sana

   
  • Chef Rahma says:

   hongera

    
 4. mashayo says:

  Delicious lazma nipike hii ungawa co mpenz wa bamia ila inanifanya nizitamani

   
 5. Joyce says:

  pishi zuri sana hili na lina virutubisho vizuri, nitalipika kwangu pia

   
 6. spacious invisible says:

  Mimi nilizoea mboga hii kwa wali nanaipendelea zaidi isipokuwa nilikuwa naongeza bilinganya ,karoti, na nyanya chungu hakika inapendeza nitamu sana

   
 7. grace says:

  Asanteee Dada kwa Haya mapishi ,mungu akubariki ,ni mazuri sana.

   
  • Chef Rahma says:

   Asante Grace

    

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*