jinsi ya kupika kabichi kwa mayai

jinsi ya kupika kabichi kwa mayai

Habari mdau wa jinsi ya kupika. karibuni tena katika jiko letu. Leo tuandae mboga ya kabichi. Mboga hii yaweza kupikwa kwa nyama, njegere, yenyewe tu kwa viungoviungo, na aina tofauti tofauti, lakini sisi leo tuipike na mayai, ni nzuri sogea karibu tuandae wote.

Mahitaji

 • kabichi 1
 • mayai 4
 • mafuta robo
 • vitunguu 4
 • nyanya 5
 • karoti kubwa 1
 • pilipili manga kiasi
 • chumvi kiasi kwa ladha

Jinsi ya kupika kabichi hatua kwa hatua

 1. Andaa kabichi ulikatekate kisha ulikoshe.
 2. libandike jikoni liive kidogo. kisha liweke pembeni.
 3. menya nyanya, kata vitunguu na karoti uviweke tayari kwa mapishi.
 4. bandika sufuria jikoni utie mafuta, yakipata moto tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi kisha tia nyanya ukaange.
 5. tia karoti kaanga kidogo, tia kabichi, pilipili manga na chumvi, vunja mayai uyapige uyatie. koroga hadi likauke, hapo linakua tayari.

Namna hiyo kabichi letu liko tayari, linakwenda sambamba na ugali, wali na hata pilau simbaya. Hivi karibuni mungu akipenda tutaandaa kabichi la njegere. karibuni sana


 

21 Comments

 1. glory dismas says:

  hapo ukila lazima mpishi Aulizwe jina

 2. Mafuta Robo lita mbona mengi sana

 3. Ahxante nami nitajarbu nahis ni tam xana

 4. atkah robert says:

  Jamani nami m nataka kujua chf ukishatia yai unalikuroga au ling’ang’aniane

 5. Vallentina Chaya says:

  Kiukweli nimejaribu ni tamu sana.

 6. haliumizi
  tumbo

 7. Mko vizuri napenda sana kipindi hiki

 8. Kesho nitapika nione utamu wake coz nahisis ni tamu sana.

  asante chef kwa maelekzo.

 9. anonciata mbilinyi says:

  hili kwakweli ni bonge la pishi nimejaribu leo .asante kwa kutuelimisha

 10. unajua kupika lakini haujasema kabeji uliichanganya wapi maana tumeichemsha tu

 11. Kwa kweli sina hadi nitakapojaribu kupika. Linaonekana nizuri.
  Ahsante kwa maelekezo.

 12. jamani,watu kwa kubuni.hongera sana mnajua sisi tutajifunzafunza

 13. nuni lema says:

  safi sana nitaenda kupika

 14. Peace Apolinary says:

  Ni vizuri kutuelimisha mapishi Mbali mbali,Asante.

 15. ashaherezi says:

  Nashkuru sana kwa kuelewa

 16. Peace Apolinary says:

  Asante kwa kuelimisha Jamani.

 17. Ahsante chef kwa mapishi mazuri

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*