Jinsi ya Kupika Kunde Mbichi za Nazi

Haloo Habari za leo tena, Karibu tupike Kunde mbichi za nazi. Mboga hii tamu ni rahisi kuandaa na ni ya gharama nafuu,lakini ina virutubisho vingi sana. karibu jikoni

Pishi: Kunde Mbichi kwa Nazi

Mahitaji

 • Kunde Mbichi Vikombe vinne (4)
 • Tui la nazi vikombe viwili (2)
 • Vitunguu Maji viwili (2)
 • Vitunguu Swaumu (Garlic) kijiko kimoja (1) cha chai kilichosagwa
 • Nyanya ya kopo nusu kijiko (1/2) cha chai
 • Pilipili Mbichi mbili(2)
 • Pilipili Hoho (pilipili mboga) nyekundu nusu (1/2)
 • Mafuta Robo (1/4)kikombe
 • chumvi kiasi

Jinsi ya kupika Kunde Mbichi hatua kwa hatua

 1. Osha vizuri kunde mbichi.
 2. Weka sufuria jikoni na chemsha maji kiasi
 3. Mimina kunde katika sufuria ya maji yanayoendelea kuchemka, Acha mpaka kunde ziive;Zikishaiva ipua kunde kisha ziweke pembeni;
 4. Mimina mafuta katika sufuria hadi yachemke kisha uweka vitunguu maji vilivyokatwakatwa kisha kaanga kiasi.
 5. Tia vitunguu swaumu huku ukiendelea kukaanga hadi mchanganyiko wako uwe kahawia (hudhurungi).
 6. Weka nyanya ya kopo katika mchanganyiko huo kisha ikaange kwa muda kiasi. Mimina kunde katika mchanganyiko huo na kisha weka Tui la nazi na acha ichemke kwa dakika kadhaa.
 7. Kisha tia chumvi kiasi na uache zichemke na kuchanganyika vizuri mpaka ibaki rojo rojo kiasi.
 8. Pakua mboga yako ya kunde mbichi za nazi tayari kuliwa.

Dondoo:

Pishi hili la kunde mbichi ni tamu sana kuliwa kwa wali.

 
 

No Comments

 1. layla mohamed says:

  kamma sina kunde mbichi naweza kutimia za kunde ya kopo?

   
  • Chef Rahma says:

   Kama hizo kunde Hazijapikwa waweza tumia. Kama zimekwishapikwa zinaweza zikaharibu ladha na mvuto wa pishi hili.

    
 2. Ashura says:

  naomba ktoka nje ya mada kidogo je wawez pika pishi hili kwa kutumia maharage

   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*