Njegere za Nazi

Njegere za Nazi

habari za muda wapenzi wa blogu yetu ya Mapishi. leo tutapika njegere za nazi, njegere zinaweza kupikwa kwa namna tofauti tofauti, unaweza kuzitia kwenye wali, pilau, unaweza kuzipika na nyama na hata kwenye tambi hupendeza. leo njegere zetu sie tutaziunga kwa kutumia nazi.
Pishi: Njegere za Nazi

Mahitaji

 • njegere nusu kilo
 • nazi 2
 • nyanya 4
 • karoti 1
 • pilipili hoho 1
 • kitunguu maji 1
 • thoum kiasi
 • mafuta ya kupikia kiasi
 • chumvi kiasi

Jinsi ya kupika njegere za nazi hatua kwa hatua

 1. chambua njegere, zikoshe, kisha zitie kwenye sufuria na maji uzichemshe ziive kiasi lakini zisilainike sana.
 2. safisha nyanya uzimenye na kuzikata. Pia katakata hoho, karoti na vitunguu. Twanga vitunguu thoum. kisha kuna nazi uchuje tui zito na jepesi.
 3. bandika sufuria jikoni, weka mafuta ukaange vitunguu, vikishabadilika rangi tia hoho kaanga kidogo kisha utie thoum na nyanya pamoja na karoti, endelea kukaanga.
 4. mimina njegere, tia chumvi na umimine tui jepesi, wacha lichemke. kisha tia tui zito liache lichemke kiasi na uzito wa njegere ukiwa sawa, tayari epua.

njegere hizi zinapendeza kuliwa na wali, ukipata kachumbari na juisi pembeni bila kusahau nyama za kukaanga hunoga zaidi. karibuni

 
 

No Comments

 1. meg says:

  Hivi tangawizi inaweza ungwa ktk nazi?

   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*