Mchuzi wa Nyama ya Kusaga

Habari ya leo wadau wa jinsi ya kupika. Karibuni tena jikoni tuandaeandae vitu vizuri, leo ni mchuzi wa kima au mchuzi wa nyama yakusaga. Ni kitoeleo kizuri cha wali, mkate, chapati na hata maandazi.

Mahitaji

 • Nyama ya kusaga nusu kilo
 • vitunguu robo kilo
 • nyanya 6 kubwa
 • viazi mbatata robo kilo
 • mafuta nusu kikombe
 • thoum kiasi
 • hiliki kidogo
 • mdalasini kiasi
 • bizari nzima kiasi
 • chumvi nusu kijiko
 • tangawizi nusu kijiko

Kuandaa Mchuzi wa Nyama ya Kuasaga Hatua kwa Hatua

 1. Osha nyama uitie kwenye chujio ivuje maji
 2. kata vitunguu, nyanya, menya viazi uvikate vyembamba
 3. menya thoum usage, saga na viungo vyote vilobakia
 4. teleka sufuria tia samli, ikichemka tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi viwe vya hudhurungi, kisha tia viazi na nyanya. Baadae tia viungo ulovisaga vyote pamoja na nyama
 5. endelea kukaanga kidogo na kisha utie maji pamoja na chumvi na limao. Acha ichemke mpaka karibu ya kukauka. Hapo itakua tayari.

Namna hiyo tutakua tumeshaandaa mchuzi wetu wa nyama ya kusaga, natumai mmelielewa na kulifurahia. Huu mchuzi waweza utoelea chapati, maandazi, mkate, ila kwa wali unaenda vizuri. Karibuni sana

 
 

No Comments

 1. nil says:

  Hivyo viazi havivurugiki? au ndio inasaidia chuzi kuwa diko diko? maanake mpaka hiyo nyama iive viazi si vitakuwa vilishakuwa uji uji au?

   
  • Salma Chef says:

   Oh havivurugiki mno ndugu yangu. Nyama yakusaga huivaharaka.

    

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*