Jinsi ya Kuandaa Chatne ya Bagia

Za muda ndugu zangu, leo tuandae kitu cha kuchapuzia bajia. Hii ni chatne ya nazi, maarufu na inakupa hamu ya kula bajia zako, ziwe za dengu au zile bajia za kunde ( vikababu)

Mahitaji

 • nazi 1
 • pilipili mbichi 3
 • ndimu kiasi
 • chumvi kiasi

Kuandaa chatne Hatua kwa Hatua

 1. kuna nazi halafu uisage iwe laini sana
 2. saga pilipili na chumvi kisha changanya vyote pamoja kwenye nazi
 3. kamulia ndimu yako, chatne tayari

chatne yetu yaweza liwa kwa bajia, kachori, na hata kababu ambazo tutawaletea matayarisho yake siku sinyingi. wadau msiache kutoa maoni na kuuliza pale panapohitaji ufafanuzi zaidi. Asante

 
 

No Comments

 1. umrat says:

  asante sana ,ila pia unaweza kutia tangawizi kidogo,pili pili ,chumvi,embe mbichi unaikata kata bila ya kuimenya ,kitunguu thomu kidogo na pilipili boga pia unasaga pamoja na nazi yako ohooooo apo bagia zinateremka tu

   
 2. michi says:

  Zur sana

   
 3. daisy says:

  Naipenda sana

   
 4. umdat says:

  Ni nzuri sana

   
 5. rahma dickson says:

  Naomba mnipe maelekezo jinsi ya kutengeneza keki kwa ujumla maana ninapojaribu huwa inalegea haikazi vizuri.

   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*