Jinsi ya kupika uji wa viazi vitamu

Jinsi ya kupika uji wa viazi vitamu: Shukurani nyingi kwa Mama Salmin mpenzi wa blogu hii kwa kututumia pishi hili. Je unajua kuwa waweza pika uji mtamu kwa kutumia viazi? fuatilia…

Pishi: Uji wa Viazi vitamu

Maandalizi

Mahitaji

 • Unga wa viazi vitamu kijiko cha chakula 1.
 • Unga wa soya kijiko cha chakula 1.
 • Unga wa mahindi vijiko vya chakula 4.
 • Limau 1
 • Sukari vijiko vya chai 2.
 • Maji vikombe 6

Utayarishaji na upishi

jinsi ya kutengeneza uji hatua kwa hatua

 1. Weka chombo safi cha kupikia jikoni, tia vikombe vitano vya maji acha yachemke.
 2. Changanya unga wa soya na unga wa mahindi kwa kutumia kikombe kimoja cha maji kilichobaki ili kufanya uji mzito.
 3. Weka mchanganyiko wako huo kwenye maji yanayochemka huku ukikoroga kuzuia unga kushikana na kuwa mabonge. Kisha acha uchemke kwa dakika kama 20.
 4. Wakati sufuria ikichemka, tengeneza juisi ya limau
 5. Baada ya dakika 20 Uji uliopikwa utakuwa mzito, ondoa uji kwenye moto na ongeza juisi ya limau na sukari.
 6. Poza, tayari kwa matumizi.

My rating 4 stars:  ????? 1 review(s)

Jinsi ya kupika uji wa viazi vitamu: Vidokezo

 • Maziwa yanaweza kuongezwa ikibidi,
 • Waweza kutumia unga wa ulezi, mtama au Muhogo badala ya unga wa mahindi.
 • Muda halisi wa kuiva uji huu inategemea na ukali wa moto na aina ya unga unaotumia.

Hilo ndilo pishi letu la leo, jinsi ya kupika uji wa viazi vitamu na soya kama lilivyoandikwa na msomaji wetu. na wewe waweza kutuma pishi lako hapa, na sisi tutalichapisha. Asante! waweza tuma maoni yako hapo chini

 

 

 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*