jinsi ya kupika chapati za maji

jinsi ya kupika chapati za maji

Jinsi ya kupika Chapati za Maji

Jinsi ya kupika Chapati za maji: Leo ninakuletea hatua kwa hatua namna ya kuandaa na kupika Chapati laini za Mayai. Tafadhali fuatana nami katika pishi hili.

Pishi: Chapati za maji/laini

Utangulizi: chapati ni kitafunwa au chakula kinachopendwa na wengi. Kuna Chapati za Kusukuma na Laini au za maji. Aina hii ya pili hupendwa zaidi na watu kwa sababu ni rahisi kutayarisha. Fuatana nami hatua kwa hatua namna ya kuandaa pishi hili tamu

Mahitaji

 • Ngano 1/2 kilo
 • mayai 3
 • mafuta au samli 1/4 kikombe
 • kitunguu kikubwa kilichosagwa 1
 • Kitunguu Swaumu punje 4
 • Chumvi 1/2kijiko au kulingana na matakwa yako

Mahitaji

Namna ya kupika chapati za maji

 1. Chekecha unga wako vizuri weka katika bakuli safi.
 2. Tia maji katika bakuli la unga na ukoroge mpaka upate uji wa wastani si mzito san a wala si mwepesi sana.
 3. Ongeza mayai na chunmvi endelea kukoroga.
 4. Ongeza kitunguu swaumu na kitunguu maji. Injika kikaango chako jikoni subiri kipate moto.
 5. Chota pawa moja mimina na tandaza kuzunguka kikaango subiri sekunde tano hadi kumi mpaka ikauke kisha geuza upande wa pili.
 6. Tia mafuta huku ukigeuza na kuzungusha ili mafuta yaenee pande zote na ili chapati isiungue. Endelea kugeuza mpaka iwe rangi ya kahawia.
 7. Hapo chapati zitakua tayari kwa kuliwa.
 8. Fanya hivyo kwa chapati zote zilizobakia

Matayarisho hayo yanatosha kupika chapati za mayai/laini sita (6) mpaka kumi (10) . Chapati za maji hupendeza zaidi kuliwa Michuzi mizito, Chai na kadhalika. Nenda kajaribu kuandaa pishi hili kisha uje utupe mrejesho. Kama una maoni yoyote kuhusu Jinsi ya kupika chapati za Maji na Mayai andika hapo chini. Asante


 

29 Comments

 1. Jamn nimejarbu zinaganda kwenye kikaango tatizo nin

 2. Hapo umatumia maji ya vuguvugu au baridi?

 3. linda choka says:

  chef mbona zangu zimekua nene!nasio laini

  • Chef Rahma says:

   Pole Linda! Jaribu kupunguza wingi wa Unga wakati wa Kupika yaani usijaze sana upawa na hakikisha unasambaza vizuri juu ya kikaango chako.

 4. Sasa sio kwamba uchanganye mayai na unga kwanza ndo utie maji maana njia yako nimejaribu zikatoka tepetepe kama mayai hayaja kolea

 5. mimitu2009 says:

  safi sana kwa elimu

 6. ni nzuri sana

 7. chapati tamu sana.Asante kwa somo zuri

 8. nimefurahi sana kwa darasa

 9. As ante kwa elimu

 10. sasa hapa unavyoweka kitunguu swaumu na kitunguu maji maana ninaona chapati inaivya vitunguu bado.

 11. james benjamin says:

  asante imenisaidia kula chapata zangu leo ……..mimi na my babieee

 12. sukari haitakiwi kwa maana kuna watu huweka VP apo??

 13. Peace Apolinary says:

  Ni mzuri sana

 14. Asante sana kwa pishi zuri la chapati za maji, nimelifurahia na nitajaribu kupika niifurahie zaidi. Ila naomba usisahau kututumia na hiyo kurasa ya viungo kwani tunapata shida mno.

  liz

 15. Chief kiukweli chapati ni tamu sana.hebu endelea kutupatia ujuzi maana yake.mafanikuo ndanu ni mazuri.

 16. Suleiman Kupaza says:

  Asante sana Che Rahma, nimepika chspati leo nyumban kwng na nimezifurahia na nimeshiba. Asante sn.

 17. nahitaji kujua kiungo kinachoitwa thom na ikiwezekana mtumie kutoa na picha za viungo

 18. nimejifunza na nimeandaa leo zimetoka poa sana ila mkitumia majina magumu ya viungo mnatupa tabu…..

 19. nashukuru kwa pishi hili nimejifunza kitu ila sijaelewa thomu ni kiungo gani mm sikifahamu au inawezekana nafahamu kwa jina lingine naomba unisaidie chef

 20. HALLO UKHT RAHMA
  MIMI HUPENDA SANA CHAPATI
  TUWEKEE NA CHAPATI ZA KUSUKMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*