jinsi ya kupika donats (dought nuts)

jinsi ya kupika donats (dought nuts)

Jinsi ya kupika Donats: Karibuni tena wadau wa jinsi ya kupika. Leo tuandae donats, hiki ni kitafunwa kipendwacho na wengi. Donats zinapendeza zikisindikizwa na chai, maziwa, kahawa, juisi na hata maji. Haya sogea karibu uweze kufatilia hatua kwa hatua.

Mahitaji

 • Unga wa ngano kilo 1
 • siagi robo kilo
 • mafuta ya kupikia lita 1
 • sukari ilosagwa robo kilo
 • maziwa robo lita
 • kungumanga kijiko 1 cha chai (ukikosa tumia mdalasini ulosagwa )
 • mayai 3
 • baking powder kijiko 1 kikubwa

[/recipes]

Jinsi ya kutengeneza Donats hatua kwa hatua

 1. Changanya unga na baking powder pamoja na siagi hadi unga uchanganyike
 2. tia sukari kidogo, kungumanga na yai kisha endelea kuchanganya unga. Weka maziwa na kanda mpaka upate donge laini
 3. tengeneza madonge, uanze kusukuma unga kiasi cha sentimeta moja. Usiwe mwembamba sana kama wa chapati.
 4. kata duara kwa glasi au kikombe kisha kata duara lingine dogo katikati kwa kutumia kifuniko cha chupa ya maji au kitu chochote chenye duara dogo, upate shepu ya ringi.
 5. Bandika mafuta jikoni, yakipata moto tia donats uzikaange mpaka ziwe na rangi nzuri, zikishaiva epua, zichuje mafuta kisha garagiza kwenye sukari ilosagwa kabla hazijapoa
 6. zitoe uziweke kwenye sahani tayari kumfikia mlaji

Haya wapenzi, hivyo ndivyo jinsi ya kuandaa donats zetu, natumai umefuatilia hatua kwa hatua. Karibuni sana”

4.0
stars based on
35
reviews Prep time:
30 Dakika
Cook time:
45 dakika
Total time:
Saa 1 n Dakika 15
Yield:
1 9" pie (10 servings)


 

Maoni 21

 1. shania Thabiti anasema:

  na ukitaka kutengeneza donati za mayai unafanaje

 2. Cintah anasema:

  oohh..nimependa pishi la leo..nina swali dogo tu,
  hivi donats hazihitaji Amira???

 3. Je unaacha unga mpka umuke ndio uanze kukaanga?

 4. peresia elinaza anasema:

  Nimependa sana pishi

 5. clesiah anasema:

  Jamani sukar ya kusaga ndio unasagaje

 6. Du nimejaribu ni Tamu sanaaaaa

 7. **namba ya simu** Mnijulishe kitabu kikiwa tayari

 8. Nauliza hivi siagi ktk kupika donat ni lazima? je nikikosa siagi siwezi pika hivijivi?

 9. hamira hua haiwekwe!!!

 10. nashukuru nimeelewa na nimepata mwanga zaid

 11. irenecharles anasema:

  unapochanganya sukari inakuwa jikoni au nijuze jamani

 12. macka ally anasema:

  asanten sanaa kwamaana nlikuwa nataman kujua donat

 13. Kassim Senjele anasema:

  ile siagi inapashwa. na vp kuhusu yale maziwa yanakandiwa kawaida bila kupashwa?

 14. Nashauri muweke mapishi haya katika apps kwa lugha ya kiswahili kama hivi

 15. ASANTE………

 16. KIBIBI KHAMIS MOHAMED anasema:

  Naomba nijue MAANA YA kungumanga

  • Salma Chef anasema:

   Ni tunda, kwa kiingereza huitwa nutmeg, ambalo hukaushwa na kusagwa, hutumika kama kiungo (spice). Kwenye donati ukilikosa waweza tumia unga wa mdalasini kiasi.

Una Jambo? Toa Maoni Hapo Chini