Jinsi ya kupika Mkate wa Mayai

Jinsi ya kupika Mkate wa Mayai

Jinsi ya kupika mkate wa mayai: Karibu tupike mkate.

Pishi: Mkate wa mayai

Maandalizi

Mahitaji

 • Mayai manne
 • Sukari vijiko viwili na nusu
 • Unga wa ngano vijiko sita vya chakula
 • Hiliki Nusu kijiko cha chai (iliyosagwa)
 • Backing powder Nusu kijiko cha chai

Utayarishaji na upishi

Jinsi ya kupika mkate wa mayai hatua kwa hatua

 1. Chukua bakuli safi, weka ndani yake sukari na hiliki, kisha vunja mayai yote juu yake.
 2. Changanya mayai, hiliki na sukari, kwa kutumia mashine (cake mixer), mpaka sukari ivurugike na mayai yapande juu kama povu.
 3. Paka mafuta chombo chako cha kuokea mkate na washa jiko (300-350f oven) lianze kupata moto.
 4. Tia baking powder katika unga wako,kisha chukua mwiko na uanze kutia unga kidogo kidogo katika mchanganyiko wako wa mayai na sukari. hakikisha unaukoroga vizuri kila utiapo unga ili kuepusha kuwa na madonge.
 5. Mimina mchanganyiko wako katika chombo cha kuchomea mkate.
 6. Oka mkate wako ndani ya jiko (oven) kwa muda wa kama dakika 20 kisha utoe.
 7. Wacha mkate upoe kisha utoe na uweke kwenye sahani safi tayari kwa kuliwa.

My rating 5 stars:  ????? 1 review(s)

Jinsi ya kupika mkate wa mayai: Vidokezo

 • Unaweza kutupia zabibu kavu juu ya mchanganyiko wako kabla ya kuoka ili kuongeza ladha (Kwa pishi letu hili Zabibu kavu robo kikombe inatosha).
 • Kuhakikisha mkate wako kama umeiva vizuri, Ingiza kijiti (toothpick) katikati ya mkate kisha kitoe. Kama ukigusa kijiti na unaona ni kikavu, basi ujue Mkate wako umeiva. Kama kuna ubichi basi mkate wako bado haujaiva.
 • Kama mkate haujaiva baada ya kukagua rudisha mkate kwa dakika 5 nyingine kisha ukague tena
 • Sukari ikiwa nyingi mkate wako utanata na hautowiva vizuri

Una maoni jinsi ya kupika mkate wa mayai? Changia hapo chini Asante


 

16 Comments

 1. Nadhani upishi wa Chapati ni tofauti Na mkate..

 2. Deogratius Emmanuel says:

  Naweza kutumia kifaa cha kuchomea chapati kuuandaa mkate huo?

 3. No maji

 4. asante sana kwa darasa zuri Mungu akulipe kheri, naamini sikukuu hii nitaandaa mwenyewe msosi wangu.

 5. Umesema mayai ma4 vijiko 6 vya kula je mayai 10, 12 je unga kilo ngapi?

 6. Stella Smith says:

  Thank you

 7. umu rahsal says:

  uko poa tnx kwa kutufunza mungu atakubariki

 8. Hamida Abubakar says:

  Samahani,unamaanisha nini unaposema vijiko visita Vya chakula?

 9. Ahsante kwa mapishi’ vijiko vya chakula tunavyotumia kula chakula? Asante

 10. Enter your comment here…nashkuru nimejifunza mkate w mayai ila nikiutia kwenye jiko unarudi tatizo n nini

 11. Mm nnapo wakt w kuchoma huwa unarud chini tatizo n nni?

 12. halmat yusuph says:

  Napenda sana Kuja kupika huu mkate wa mayai ni me furahi sn

 13. Ahsante tunajifunza vingi kupitia hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*