Jinsi ya Kupika MKATE WA UFUTA

Vipi hali zenu wadau wa mambo yetu ya jikoni, Leo tukutane tuandae mkate wa ufuta. ni kitafunwa kizuri sana katika mlo wa asubuhi na hata jioni ukipata na kinywaji cha moto pembeni.

Mahitaji

 • unga wa ngano kilo1
 • nazi kubwa 1
 • ufuta kiasi
 • chumvi kiasi
 • samli robo kilo
 • hamira kiasi

Jinsi ya Kuandaa na kupika Mkate wa Ufuta

 1. kuna nazi, ichuje upate tui zito.
 2. chukua unga, uuchanganye kwenye tui la nazi, weka hamira na chumvi kwenye huo mchanganyiko. uvuruge mpaka ulainike, usiwe mzito mno wala mwepesi mno
 3. Acha Mchanganyiko wako uumuke kwa nusu saa,( itategemea aina ya hamira yako), ukishaumuka weka kikaango kwenye jiko lako la mkaa, kikipata moto vizuri kinyunyizie maji.
 4. kata donge la unga uliweke kwenye kikaango. Tandaza kwa vidole mpaka liwe duara. chukua ufuta unyunyizie juu yake.
 5. subiri kidogo ugandie kwenye chuma, kisha geuza chuma juu chini ili uso wa mkate upate moto mpaka ubadilike rangi, hapo unakua ushaiva. Ubandue kwa kutumia kisu uuweke kwenye sahani, uunyunyizie samli iloyeyushwa.
 6. endelea kuichoma mikate mengine mpaka unga wote uishe.

Naam, mikate yetu ya ufuta yapendeza ikiliwa na kinywaji ukipendacho, iwe chai, maziwa, juisi na hata upate rosti la nyama pembeni yake hunoga. Wadau kwa maswali na maoni msisite kututumia. Asanteni

 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*