Jinsi ya Kupika Vitumbua vya Nyama

Jinsi ya Kupika Vitumbua vya Nyama

 • Leo tena vitumbua, lakini hatutamia unga wa mchele kama tulivyozoea, bali nyama ya kusaga. Ni pishi zuri sana, ukiwa na juisi pembeni, vinapendeza sana kula muda wa jioni, ila waweza kula muda wowote wa nafasi yako. Haya jiweke tayari tuanze kuandaa pishi hili Tamu.

Pishi: Vitumbua vya Nyama

Mahitaji

 • Nyama ya kusaga robo
 • Kitunguu 1
 • Kitunguu thoum nusu kijiko
 • Karoti 1
 • Pilipili hoho nusu
 • Mayai 5-6
 • Baking powder nusu kijiko kidogo
 • Pilipili manga kiasi
 • Pilipili mbichi(ukipenda)
 • Chumvi kiasi

Namna ya kupika vitumbua vya nyama Hatua kwa hatua

 1. Safisha nyama, uitie thoum, chumvi, pilipili manga na tangawizi, ibandike jikoni ili iive na ikauke vizuri
 2. kata vitunguu, hoho, pilipili na uvichanganye na mayai, kisha vyote vitie kwenye nyama yetu
 3. Weka kwenye blender mchanyanyiko wetu uusage kidogo ila usiwe laini sana. Ikiwa tayari, mimina katika bakuli.
 4. Kisha tia baking powder, karoti na chumvi kidogo kisha changanya vizuri.
 5. andaa chuma cha kukaangia vitumbua, bandika jikoni, weka mafuta kidogo.
 6. Mafuta yakipata joto chota kwa upawa mchanganyiko wetu utie kwenye kikaango, vikiiva upande mmoja geuza na upande wa pili uive kisha uvitoe.
 7. Endelea kuchoma hadi viishe vyote, hapo tunakua tumemaliza upishi wetu wa vitumbua

Natumai tumeenda sambamba hatua kwa hatua jinsi ya kupika vitumbua vya nyama. Karibuni kwa maoni, maswali na ushauri hapo chini.

 
 

No Comments

 1. Halima says:

  Habari wapendwa, napenda kutoa shukrani ya pekee kwa waandaji na wamiliki wa blog hii kwani inatufundisha mambo mengi ya jikoni ambayo ni faida katika familia zetu. Pishi hili limekaa vizuri big up!

   
  • Salma Chef says:

   Shukrani, karibu tena

    
  • Salma Chef says:

   Asante sana kutembelea blog yetu.

    
 2. mwanaidi says:

  Ni zuri ngoja nikapike leo halafu nitarudi kutoa matokeo.

   
  • Salma Chef says:

   Jaribu mdau, ni nzuri utuite tukuonjee

    
 3. joyce says:

  I will try this aiseee

   
  • Salma Chef says:

   Joy jaribu mpendwa, usisahau kutupa mrejesho mwaya

    
 4. mama k says:

  Wow…. Nimefurahi kuijua blog hii. Msichoke kutufunza. Nawapenda

   
 5. Shufaa says:

  Wow mapishi mazuri na yameelezwa vizuri kwa lugha yakueleweka nimependa sana mapishi yenu endeleeni kutufunza .

   
 6. Beatrice josiah says:

  Naitwa Beatrice aiseeee nimependa hii acha nijarbu

   
 7. joha senga says:

  Nlikua cjui kama Kuna vitumbua vya nyama, Ashante da Salma

   
 8. niite mamy'G' says:

  Dada yangu ww ahsante kwa kunipa mwanga, mara nyingi nimewahi kula vitumbua hivi harusini, navipenda sana ila ckujua vinapikwaje, siku moja nilijaribu kupika ila vilikuja vinne tu tena kwa shida sana, vilivyobaki vyote vilivurugika na havikushikana hadi nikabadilisha mapishi. sasa nimelijua kosa langu na sitokosea tena kupitia maelekezo yako. Ahsante Dada kwa msaada wako na Mungu akubariki.

   
 9. Amria says:

  Asante nimejarib it’s good taste ?

   
 10. Amria says:

  Kuna pishi linaitwa fish triangle unalijua

   
 11. yasinta says:

  nimefurahi sana na nimejifunza kupika, naomba kunifundisha namna ya kupika kababu.

   
  • Chef Rahma says:

   Asante Yasinta.. Kwa mapishi ya Kababu
   Angalia Hapa Mapishi ya kababu

    

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*