Jinsi ya Kupika Katlesi za Samaki

Jinsi ya Kupika Katlesi za Samaki

Habarini za muda huu wapenzi wa jinsi ya kupika. Jiweke tayari tuandae pishi letu la leo, katlesi za samaki. Ni miongoni mwa chakula kipendwacho na wengi kutokana na ladha yake. Haya sasa natumai upo tayari tuandae pamoja.

Mahitaji

 • samaki vipande viwili
 • viazi mbatata(mviringo) nusu kilo
 • mafuta lita 1
 • ndimu 2
 • vitunguu thoum
 • tangawizi
 • mayai 2
 • pilipilimanga ya unga
 • mdalasini wa unga kiasi
 • chumvi kiasi
 • uzile (bizari nyembamba) wa unga

Namna ya kuandaa na kupika Katlesi za samaki

 1. Osha viazi, vichemshe mpaka viive, kisha viache vipoe
 2. Menya viazi na uviponde viwe laini
 3. Msafishe samaki, mtie chumvi, thoum, tangawizi, pilipilimanga, mbandike jikoni akauke vizuri
 4. mchambuechambue samaki wako
 5. changanya samaki na viazi, chumvi, uzile, mdalasini, pilipilimanga, thoum, tangawizi, kamulia na ndimu.changanya vizuri
 6. Fanya vidonge vidonge vyenye umbo zuri
 7. piga mayai kwenye bakuli
 8. chovya katlesi kwenye mayai na kaanga kwenye mafuta ya moto. Tumia karai kukaangia
 9. ukipenda garagiza kwenye unga wa tosi kabla hujazikaanga
 10. zikishaiva, zitoe uzichuje mafuta, kisha uzitie kwenye sahani tayari

Naam, katlesi zetu za samaki tumeziandaa namna hiyo, karibuni


 

6 Comments

 1. Mashaallah Mashaallah Mashaallah Chef Salma..mimi mgeni kwa site ya mapishi yako na Nina furaha sana kupata mapishi yako na jifunza mengi.JazakAllah kheir

 2. Asante sana kwa mafunzo kamili. Mungu aibariki kazi yako.

 3. Nimevjaribu kuchanganya na samaki viazi vimelainika kiasi cha kwamba vinanata na imekua ngumu kutengenezeka shape ya aina yeyote,naomba msaada

  • Chef Rahma says:

   Pole sana ikitokea hivyo unaweza kuweka ngano kidogo wakati wa kutengeneza shape. Hakikisha unachemsha viazi pamoja na maganda yake ili kuepusha kulainika kupita kiasi asante

 4. Mhhh asante, nimepatamlo wangu wa jioni hii…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*