Jinsi ya kupika Sambusa za nyama

Ndugu wapenzi, Leo tunakuja na Jinsi ya kupika Sambusa Za nyama. Sambusa  Hupendwa na wengihasa za nyama. Sambusa ni Tamu sana, wengi hupenda kula pamoja na Juisi, soda na hata chai.

Mapishi ya Sambusa Za Nyama /Jinsi ya kupika sambusa hatua kwa hatua

Mahitaji

 • ½ kilo Nyama ya iliyosagwa
 • kijiko 1 kikubwa cha chakula cha Pilipili manga
 • Kijiko kimoja cha chakula cha kitunguu Thomu na tangawizi iliyosagwa
 • Mafuta ya kupikia Kiasi
 • Vijiko vinne unga ngano au ute wa yai kwa kufungia sambusa
 • Kaki za sambusa/manda/ chapati nyepesi (unaweza kununua zilizokuwa tayari zimeshakatwa kwa ajili ya sambusa au kama utanunua zile sheet pana utazikata kwa inchi 4 upana wa ruler yaani upate mistari 3

Directions

 1. Kausha nyama ya kusaga kwa kiyunguu swaumu (thomu) na tangawizi pamoja na chumvi mpaka ikauke vizuri Iwache ipoe.
 2. Kata kata majani ya kotmiri weka upande Kata kata upate vipande vidogo vidogo(chop) vya vitunguu maji.
 3. Zikate pili pili zako slice za mviringo vidogo vidogo.
 4. Wakati ukimaliza matayarisho haya na nyama yako itakuwa ishapoa kabisa hapo ndio utachanganya,bizari nzima pamoja na pilipili manga pamoja na vitu vyote ulivyokwisha vitayarisha
 5. Koroga unga ndani ya kibakuli au ute wa yai
 6. Weka kaki kwa mfungo wa triangle yaani pembe tatu kama kofia na
 7. weka mchanganyiko wa nyama yako kiasi na uanze kuzifunga sambusa zako na ukifika mwisho hapo ndipo upake unga wako kwa ajili ya kuifunga isifunguke wakati wa kuchoma, pendelea kutumia kaki 2 kwa kila sambusa moja.
 8. Kuchoma kwake ikiwa unazifanya na kuzichovya hapo hapo mafuta lazima yawe baridi (ninakusudia uweke mafuta na uzitie sambusa kabla hayajapata moto).
 9. Na ikiwa uliziweka kwenye friji zikaganda basi unatakiwa uzichome kwa mafuta ya moto

Muhimu

Watu wengi hupata usumbufu katika kufunga sambusa, Jaribu mara kwa mara utafanikiwa tu, ni kiasi cha kuzowesha mikono kufuatisha ile Triangle tu.

Pia waweza kutupia njegere kiasi zilizopikwa katika mchanganyiko wako wa nyama ili kupendezesha zaidi. Kama nilivyofanya katika sambusa zangu hapo juu.

Hivyo ndivyo Jinsi ya kupika Sambusa za nyama. Ahsanteni

 
 

No Comments

 1. Esta says:

  Mhh, zinaonekana tamu hizo,
  asante

   
 2. Neli says:

  Thomu ni nini umeizungumzia kwenye mapishi?

   
  • Chef Rahma says:

   NI VITUNGUU SWAUMU AU GARLIC KWA LUGHA YA KIINGEREZA…
   Asante sana….NELI

    
 3. sophia says:

  Asante kwa kutuelimisha

   
 4. beatrice says:

  ts gud

   
 5. Mlaga says:

  Hakika tunajifunza, Naomba nisaidie kupika biliani binafsi cjui jinsi ya kupika na napenda sana kujua, Asante kazi njema

   
 6. RUSI says:

  Ashante kwa pishi hili lakini nilikua naomba kuuliza kaki ni mini?

   
 7. beatrice says:

  mmmh nataman nijue

   
 8. Jema Ibrahim. says:

  Ahsante mi nimeipenda, ila shida ni kwamba, nashindwa kuandaa chapat ya hy sambusa

   
 9. najmaabdul says:

  Sambusa ni tamu asante kwakutufundisha

   
  • Chef Rahma says:

   Karibu. Najma

    
 10. ivanovic morgan says:

  Asante kwa msaada wako

   
 11. evelyne says:

  asanteni

   
 12. evelyne says:

  nimependaaa

   
  • Chef Rahma says:

   Asante kwa kupenda Pishi letu

    
 13. Maria says:

  Asante, but kwenye mahitaji baadhi ya vitu na kiasi vyao vimekosekana ambavyo umesema kwenye directions za kupika. Kotmiri ni nini kwa kingereza?, asante sana

   
 14. Anna Alex says:

  Ni namna gani nitafanya ili niweze kukata hy triangle, shida iko hapo

   
 15. mwema says:

  SIJAELEWA

   
  • Salma Chef says:

   Pole sana Mwema. Ni sehemu gani katika maelezo ambayo hujaielewa? tupo kukusaidia. Asante

    
 16. Mariam omari says:

  Naomba nielezwe jinsi ya kutengeneza sheets hizo za sambusa

   
 17. mwema says:

  BADO SIJAELEWA

   
 18. peresia elinaza says:

  Mbona hamjatufundisha namna ya kuukanda huo unga wa manda?

   
 19. Nuwiya Sultan says:

  Sina, naenda kujaribu

   
 20. beatrice says:

  Sasa kama napika nyingi na umesema nianze kupika mafuta yakiwa bado hayajapata moto sasa zinazofuata baada ya mpiko was kwanza itakuwaje

   
 21. John Mtulya says:

  Chef Mimi nahitaji kujua unatengenezajaze hizo sheet

   
 22. ema the boy says:

  ngoja nijalibu

   

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*