jinsi ya kupika vitumbua

Habarini wadau wa mapishi, leo nimewaandalia jinsi ya kupika vitumbua. Hiki ni kitafunwa kinachopendelewa sana kwa chai. unga utokanao na mchele ndio unaotumika.

Pishi: Vitumbua

Mahitaji

 • mchele kilo 1
 • nazi kubwa 2
 • hiliki kiasi
 • sukari robo kilo
 • hamira kiasi kijiko kimoja nusu ( itategemea aina ya hamira)
 • mafuta nusu lita
 • mayai 3 (ukipenda)

Pishi la Vitumbua Hatua kwa Hatua

 1. uroweke mchele uliokwisha uchambua vizuri na kuupeta.
 2. utandaze sehemu safi ukauke, kisha usage upate unga mlaini
 3. kuna nazi uchuje tui zito
 4. saga hiliki, changanya na sukari
 5. changanya ule unga wa mchele, sukari, hiliki, tui la nazi na hamira. uvuruge uwe mwepesi kiasi cha kuweza kuchoteka kwa upawa. Acha uumue kwa dakika 25 hadi 30 kutegeme na ubora wa hamira.
 6. weka kikaango cha kukaangia vitumbua jikoni, anza kukaanga vitumbua vyako kwa kueka mafuta kwanza yapate moto, kisha unachota kwa upawa unga na kueka kwenye vijungu vya kikaangio chetu. unaacha vichemke upande mmoja, kisha unageuza upande wa pili, vikishaiva vitoe weka kwenye chujio ili mafuta yajichuje. Endelea kukaanga viliobakia mpaka unga uishe

vitumbua hivi vinaweza kuliwa na chai, maziwa, uji na hata juice ukipenda. ukivipata bado vimoto huwa safi sana.

Jinsi ya kupika Vitumbua. Kama una maoni yatupie hapo chini Asante

 
 

No Comments

 1. JOYCE SIMBEYE says:

  MAELEKEZO YAMETULIA ILA NAULIZA HAMIRA NI KIJIKO CHA CHAI AU CHA CHAKULA

   
 2. saleh ally says:

  km mchele nusu kilo jee nazi ngapi

   
  • Chef Rahma says:

   Asante kwa kusoma pishi letu. Tumia nazi moja kwa nusu kilo. Punguza vipimo au ongeza kuwiana na kipimo cha mchele

    
 3. joyce says:

  Jamani mm ni mpenzi Wa vitumbua,lakini kila napojaribu kuvipika,ndani vinakua vitepe,huwa nakosea wapi?

   
 4. Glory S Shirima says:

  Nimependa pishi la leo,mie ni mpenzi Wa vitumbua nitajaribu na mimi.big up kwa kutuelimisha

   
 5. Makala dilunga says:

  Natakaa kujua kwann unga wa vitumbua hauwezi kukaa zaidi ya siku 3 je tatizo unga haukauki au ni nn

   
 6. Maua says:

  Je vinapatikana wapi kikarai cha vitumbua kama chako?

   
 7. dickson says:

  machele nusu viungo vingine nikiasi gani?

   
 8. dickson says:

  machele nusu viungo vingine nikiasi hani

   
  • Chef Rahma says:

   Kwa Mchele Nusu, Viungo vingine utagawanya mara Mbili. asante

    

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*